Inaelezwa kuwa Marekani iliapa kulichukulia hatua kundi hilo kutokana na “uvunjaji wa wazi wa mkataba wa amani” uliosimamiwa na Ikulu ya White House.

Kundi hilo linaloungwa mkono na Rwanda lilichukuwa udhibiti wa mji huo wa kimkakati karibu na mpaka wa Burundi wiki iliyopita, siku chache baada ya serikali za Kongo na Rwanda kusaidi mkataba wa amani mjini Washington, mkataba ambao Rais Donald Trump aliusifia kuwa “muujiza mkubwa.”

Hatua hiyo ya M23  imeutia doa mchakato huo wa amani na kuzusha hofu za vita vikubwa zaidi vya kikanda.

Kwa kuushikilia kwake mji wa Uvira uliliwezesha kundi hilo kudhibiti mpaka wa Kongo na Burundi na kuikatia serikali mjini Kinshasa msaada wa kijeshi kutoka jirani yake huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *