Bwana Salih atamrithi Filippo Grandi wa Italia, ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa dhati kwa uongozi wake na juhudi zake zisizochoka katika kuwalinda wakimbizi, watu waliolazimika kuhama makazi yao na watu wasio na utaifa.

Aamwahi kuhudumu kama Rais wa Iraq (2018–2022), na akiwa na taaluma ya zaidi ya miongo mitatu ya huduma serikalini nchini Iraq na katika Mkoa wa Kurdistan, Bwana Salih analeta uzoefu mpana wa uongozi wa kidiplomasia, kisiasa na kiutawala katika ngazi za juu, ikiwemo kushirikiana na taasisi za kimataifa na kikanda, pamoja na dira na uzoefu wa haki za binadamu na masuala ya kibinadamu, ikiwemo kama mkimbizi, mpatanishi wa migogoro na mbunifu wa mageuzi ya kitaifa. Alihudumu mara mbili kama Waziri Mkuu wa Serikali ya Mkoa wa Kurdistan (2001–2004; 2009–2012) na kama Naibu Waziri Mkuu wa Iraq (2004–2009), sambamba na wadhifa wa Waziri wa Mipango (2004–2006). Alikuwa na mchango wa msingi katika ujenzi upya na uokoaji wa uchumi wa Iraq baada ya mwaka 2003, ikiwemo majadiliano ya Mkataba wa Kimataifa na Iraq kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia.

Kwa sasa, Bwana Salih anahudumu kama Mtafiti Mwandamizi (asiye mkazi) katika Kituo cha Belfer cha Sayansi na Masuala ya Kimataifa, Shule ya Kennedy ya Harvard, Marekani, na pia kama Mshirika wa Uongozi (asiye mkazi) katika Taasisi ya Mashariki ya Kati (Middle East Institute) jijini Washington, D.C., Marekani.

Akiwa Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Marekani cha Iraq, Sulaimani (AUIS), Bwana Salih ana shahada ya uzamivu (PhD) katika Takwimu na Matumizi ya Kompyuta katika Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Liverpool, Uingereza, na shahada ya kwanza (BSc) katika Uhandisi wa Kiraia kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff, Uingereza. Mbali na lugha zake za asili za Kikurdi na Kiarabu, anazungumza Kiingereza kwa ufasaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *