Shirika la Kimataifa la Haki za binadamu limearifu kuwa Dakta Hussam Abu Safiya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kamal Adwan huko Gaza ambaye amekuwa mikononi mwa Israel tangu mwaka 2024 anakabiliwa na tishio kubwa kwa maisha yake.

Shirika la Physicians for Human Rights limeripoti  kuwa naser Odeh Wakili wa Dakta Abu Safiya ameshuhudia majeraha makubwa, viashiria vya kunyanyaswa kimwili, matatizo ya kupumua na matukio ya mara kwa mara ya kupoteza fahamu wakati wa alipomjulia hali Abu Safiya tarehe pili mwezi huu wa Julai katika eneo anaposhikiliwa la Rakefet ndani ya Gereza la Israel la Nitzan.

Wakili Nasser Odeh anasema: Abu Safiya aliletwa mbele yangu akiwa amefungwa pingu mikononi na miguuni, huku akiwa ameandamana na walinzi wa gereza waliovaa barakoa.

Wakili Nasser Odeh anaendelea kusema: Dakta Hussam Abu Safiya alikuwa na majeraja na michubuko mikubwa kuzunguka kichwa, macho, masikio na shingo yake. ” Hali ya kimwili ya Dakta Abu Safiya imedhoofika sana kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtambua, ameeleza Wakili mtetezi wa Mkurugenzi huyo wa Hospitali ya Kamal Adwan huko Gaza ambaye anashikiliwa katika gereza la Israel tangu mwaka 2024.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *