
Antonio Costa aliandika kupitia mtandao wa X akithibitisha juu ya uamuzi huo na kwamba fedha hizo zitatumia kwa mwaka 2026 hadi 2027.
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema mapema leo Ijumaa kwamba Umoja wa Ulaya umetuma “ishara ya wazi” kwa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin, kufuatia makubaliano hayo.
Ameandika kupitia mtandao wa X kwamba, huo ni ujumbe kwa Putin kwamba, Vita vyake nchini Ukraine havitakuwa na maana tena.