
Taarifa hiyo imetolewa na kituo cha utangazaji cha ABC nchini Australia siku ya Ijumaa.
Polisi wa New South Wales wamewakamata wanaume hao katika kitongoji cha Liverpool huko Sydney jana Alhamisi, wakitokea jimbo jirani la Victoria wakitumia magari mawili.
Naibu Kamishna wa Polisi wa NSW David Hudson aliiambia ABC Sydney kwamba kulikuwa na “ishara fulani kwamba Bondi lilikuwa ni moja ya maeneo ambayo huenda waliyatembelea.
Waziri mkuu wa Australia mapema leo ametangaza mpango wa kitaifa wa kununua tena bunduki ili kuziondoa silaha nzito kufuatia mauaji hayo yaliwaua watu 15 na kuwajeruhi wengine kadhaa.