Waziri Mkuu wa Ufaransa Sébastien Lecornu amefanya mkutano na waandishi wa habari mjini Paris siku ya Alhamisi, Juni 11, kuhusu kuingiliwa kwa kidijitali na nchi za kigeni katika siasa za Ufaransa. Kwa kuzingatia chaguzi sita zilizofanyika nchini Ufaransa tangu mwaka 2021, mkuu wa serikali hakuficha wasiwasi wake kuhusu hatari za uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwaka ujao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tunawezaje kuzuia nchi za kigeni kujaribu kushawishi matokeo ya uchaguzi wa urais utakaofanyika nchini Ufaransa mwaka ujao kwa kueneza maudhui ya uongo kwenye mtandao? Hii ilikuwa mada ya mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa siku ya Alhamisi, Juni 11, na Waziri Mkuu, Sébastien Lecornu, katika Sekretarieti Kuu ya Ulinzi na Usalama wa Taifa, jijini Paris.

Chini ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi ambapo atapatinaka mrithi wa Emmanuel Macron, serikali ina wasiwasi ulio wazi kuhusu hatari inayoweza kujitokeza. Na sababu: ingawa chaguzi sita zimefanyika nchini tangu mwaka 2021, hakuna hata moja ambayo imeepuka kuingiliaji kidijitali kwa nchi za kigeni. “Hatari ilikuwa kubwa katika uchaguzi wa manispaa,” Waziri Mkuu alibainisha, akielezea furaha yake kwamba “hakukuwa na athari kubwa” lakini ana wasiwasi kuhusu “matarajio ya vitisho vikubwa” ambavyo “vinaweza vikatokea […] kwa uchaguzi wa urais.”

Waziri Mkuu anatumai, haswa, kwamba sheria inayotegemea makubaliano kuhusu kuingiliwa itawekwa kwenye ajenda ya bunge msimu huu wa vuli kwa lengo la kupitishwa kabla ya uchaguzi wa rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *