Uturuki imeahidi kuendelea kushirikiana na mataifa ya Afrika ikiwemo katika mafunzo na usaidizi wa kiufundi, kwa lengo la kukabiliana na ugaidi na kuimarisha usalama katika bara hilo.

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki, Yaşar Güler, ameeleza wakati wa mkutano na wawakilishi wa mashirika ya habari jijini Ankara mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya kufanyia tathmini shughuli za wizara yake.

“Kuhusu Afrika, kuimarisha ushirikiano wetu katika masuala ya ulinzi na mataifa ya Afrika – ambayo tuna uhusiano wa kihsitoria nao pamoja na kitamaduni – na kwa hivyo kuchangia katika usalama na uthabiti wa bara hilo kunabaki kuwa miongoni mwa vipaumbele vyetu,” Güler alisema.

“Kulingana na maombi tuliyoyapokea, tunaendelea kutoa mafunzo, fedha, vifaa, na kuwaunga mkono kiufundi Majeshi ya mataifa ya Afrika, hivyo kuchangia katika juhudi za kuimarisha uwezo wao. Kwa muktadha huu ushirikiano wetu wa mafunzo ya kijeshi, tunatoa mafunzo ya lugha ya Kituruki kwa nchi 12 (Somalia, Libya, Senegal, Gambia, Burkina Faso, Cameroon, Mali, Djibouti, Nigeria, Niger, Gabon, na Guinea) kupitia wizara yetu, Wakf wa Uturuki wa Maarif, na Taasisi ya Yunus Emre.”

‘Libya yenye Umoja’

Katika juhudi za Uturuki kwa ajili ya kuwa na Libya yenye umoja, waziri alisisitiza “Uhusiano wa kihistoria wa siku nyingi” kati ya nchi hizo mbili, akiieleza Libya kama “jirani zetu wa Mediterani”, na kuhakikisha dhamira ya Uturuki kwa amani.

“Mafunzo yetu ya kijeshi, usaidizi, ushirikiano, na shughuli za ushauri nchini Libya zinaendelea kwa lengo la kuwa na Libya moja kumehakikisha kuwepo kwa uhuru wake na umoja wa kisiasa, kuishi kwa amani, utulivu, na uthabiti,” Yaşar Güler aliongeza.

“Ushirikiano wetu wa masuala ya baharini, ni msingi ambao uliwekwa kwenye makubaliano kuhusu shughuli za maeneo ya bahari yaliyotiwa saini 2019, yameimarishwa na kujumuisha sekta kama ulinzi wa nishati na kukabiliana dhidi ya uhamiaji haramu,” alieleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *