Ukraine: Mashambulizi ya anga ya usiku yaendelea kuwa jinamizi kwa ariaUkraine: Mashambulizi ya anga ya usiku yaendelea kuwa jinamizi kwa aria

Mashirika hayo yameonya kuwa ikiwa ni katikati ya majira ya baridi kali, mamilioni ya nyumba zimekosa umeme, hali inayohatarisha upatikanaji wa vipasha joto, maji na huduma muhimu.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura OCHA, mashambulizi ya anga ya Urusi yalilenga mji mkuu Kyiv, pamoja na mkoa wa Khmelnytskyi magharibi mwa nchi na mkoa wa Zhytomyr Katikati ya taifa hilo. Nyumba, miundombinu ya nishati na vifaa vya bandari pia vimeshambuliwa katika miji ya Chernihiv kaskazini, Odessa kwenye pwani ya Bahari Nyeusi, na Sumy kaskazini-mashariki, na kusababisha usumbufu mkubwa wa huduma za msingi.

“Katika maeneo mengi ya nchi, familia nyingi zinajiandaa kukabiliana na majira magumu ya baridi bila umeme majumbani mwao,” OCHA imeonya kupitia mtandao wa kijamii wa X.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Ukraine, jeshi la Urusi lilifanya shambulio jipya kubwa dhidi ya gridi ya umeme ya Ukraine kuanzia usiku jana hadi leo asubuhi ya Jumanne. 

Inaripotiwa kuwa majimbo matatu magharibi mwa nchi hiyo yamekosa umeme kwa kiwango kikubwa.

media:entermedia_image:ca62ecc3-a1e9-4a2a-af73-503d98d7dad0

Mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa akikagua moja ya majengo yaliyoharibiwa na makombora ya anga ya Urusi

Majira mengine magumu na ya kutisha kwa watoto

Athari za kibinadamu za mashambulizi haya kutoka Moscow ni za haraka. “Kadri msimu wa baridi unavyoanza, walio hatarini zaidi wanahitaji msaada zaidi. Vurugu hizi lazima zikome,” OCHA imesisitiza, ikikumbusha kuwa “raia lazima walindwe.”

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, linaripoti “habari za kusikitisha”, mtoto mmoja aliuawa na watu wengine watatu kujeruhiwa katika maeneo ya Kyiv, Vyshhorod na Zhytomyr wakati wa shambulio la usiku uliopita. Huduma za vipasha joto, umeme na maji zilikatika katika maeneo kadhaa.

“Watoto wanakabiliwa na majira mengine ya baridi magumu na ya kutisha maisha ya watoto yako hatarini.” Limeonya shirika hilo.
Simamisheni mashambulizi. Waacheni watoto wawe watoto tena,” 

UNICEF imesisitiza kupitia mitandao ya kijamii “Wakati umefika sitisheni vita kunusuru watoto na kila mtu.”

Hali ya maisha ya watu katika eneo la migogoro Mashariki mwa Ukraine. Picha hii ilipigwa kabla ya vita ya uvamizi wa sasa wa Urusi.

© UNHCR/Anastasia Vlasova

Hali ya maisha ya watu katika eneo la migogoro Mashariki mwa Ukraine. Picha hii ilipigwa kabla ya vita ya uvamizi wa sasa wa Urusi.

Wikiendi yenye vifo vingi na kulengwa miundombinu 

Mashambulizi haya mapya yanafuatia wikiendi iliyokuwa na vifo vingi, iliyoghubiwa na “ongezeko la vifo vya raia na uharibifu mkubwa wa miundombinu muhimu.” 

Kati ya tarehe 19 Desemba hadi asubuhi ya Jumatatu tarehe 22 Desemba, mamlaka za Ukraine ziliripoti vifo vya zaidi ya raia kadhaa na zaidi ya watu 70 kujeruhiwa.

Usumbufu wa huduma za msingi uliripotiwa katika zaidi ya miji na vijiji 270. Mkoa wa Odessa, ambao umekuwa ukishambuliwa karibu kila siku, uliathirika zaidi. 

Tarehe 19 Desemba, shambulio la usiku lililolenga miundombinu ya bandari liliua raia wanane na kujeruhi wengine 27, kulingana na mamlaka. 

Mashambulizi yaliyofuata yalisababisha kukatika kwa umeme kwa kiwango kikubwa, na kuathiri makumi ya maelfu ya watu.

Mikoa ya Dnipro katikati-mashariki mwa Ukraine, Kharkiv kaskazini-mashariki na Mykolaiv kusini pia ililengwa, hasa miundombinu ya nishati, na kuathiri mamia ya maelfu ya wakazi. Kituo cha afya na shule viliharibiwa. Vifo na majeruhi pia viliripotiwa katika Donetsk mashariki, Kherson kusini na Zaporizhzhia kusini-mashariki. 

Katika mkoa wa Mykolaiv, ghala lililokuwa likihifadhi misaada ya kibinadamu liliharibiwa katika shambulio la tarehe 20 Desemba.

Watoto wakiwa wamejificha ili kusaka usalama dhidi ya makombora kwenye kituo cha treni mjini Kyiv nchiin Ukraine

© UNICEF/Oleksii Filippov

Watoto wakiwa wamejificha ili kusaka usalama dhidi ya makombora kwenye kituo cha treni mjini Kyiv nchiin Ukraine

Ombi la kibinadamu ililofadhiliwa kidogo

Wakati huo huo, uhamishaji wa raia kutoka maeneo ya mstari wa mbele na maeneo ya mpakani unaendelea. 

Katika mkoa wa Sumy kaskazini-mashariki, takribani watu 40 wamehamishwa kwenda maeneo salama katika siku tatu zilizopita, kwa mujibu wa OCHA. 

Katika mkoa wa Donetsk ulioko mstari wa mbele, karibu raia 330, wakiwemo watoto takribani 50, pia wamehamishwa.

Tangu Juni, karibu watu 150,000 wameondoka katika maeneo ya mapigano, wakiwemo zaidi ya watoto 16,500 na zaidi ya watu 5,000 wenye ulemavu

Mwaka huu, wahudumu wa kibinadamu wameweza kutoa msaada kwa zaidi ya watu 700,000 wanaoishi karibu na mstari wa mbele mashariki.

Hata hivyo, mahitaji yanazidi kwa kiasi kikubwa rasilimali zilizopo. Upungufu wa ufadhili umewaacha zaidi ya watu milioni moja bila upatikanaji wa maji safi na umezuia huduma za ulinzi, hususan kwa waathirika wa ukatili wa kingono. 

Ombi la Umoja wa Mataifa la dola bilioni 2.6 kwa ajili ya Ukraine limepata ufadhili wa nusu tu, huku vita vikiendelea bila kupungua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *