
Kufuatia mashambulizi mapya yaliyoratibiwa na wanajihadi wa kiislamu na washirika wao waasi wa Tuareg nchini Mali, jeshi la nchi hiyo linaonekana kutishwa zaidi na kutengwa kuliko wakati mwingine wowote katika mji mkuu Bamako na ngome zake nyingine kwenye mji wa Kati.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ikiwa ni miezi miwili tu imepita tangu wanajihadi hao watekeleze mashambulio makubwa zaidi huko Kidal ambayo yaliwadhoofisha watawala wa kijeshi, kundi la kijihadi la JNIM lenye uhusiano na Al-Qaeda pamoja na waasi wa Tuareg walifanya operesheni nyingine ya mashambulizi siku ya Jumamosi katika maeneo tofauti ya nchi.
Mashambulizi ya wikendi iliyopita, yanathibitisha uwezo wa wapiganaji hao kuusumbua utawala wa kijeshi, ambao tangu umeingia madarakani unahangaika kudhibiti usalama kwenye maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo, licha ya usaidizi wa mamluki wapiganaji kutoka Urusi.
Waasi hao walishambulia miji kadhaa ya kaskazini na kati ikiwemo moja ya jela kubwa zaidi nchini humo iliyoko umbali wa kilometa kadhaa kusini mwa jiji kuu la Bamako.
Wapiganaji wa Tuareg, wameripoti kuudhibiti mji wa Anefis ambao una sehemu kubwa mamluki wa Urusi, mapigano yakiripotiwa hadi kusikia usiku wa Jana, waasi hao pia wakiripotiwa kushambulia msafara wa wanajeshi wa Serikali na wale wa Urusi waliokuwa wanatokea mji wa Gao kwenda Anefis.