Katika taarifa iliyotolewa mjini New York kupitia msemaji wake Farhan Haq, Katibu Mkuu amesema mamlaka husika zinapaswa kuhakikisha kuwa “uchaguzi wa rais, wabunge, wa mikoa na wa manispaa unafanyika kwa namna ya amani, yenye utaratibu, jumuishi na ya kuaminika.”

Amewahimiza wadau wote wa kisiasa kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuchochea vurugu au kudhoofisha uaminifu wa mchakato wa uchaguzi, akisisitiza umuhimu wa “kulinda utawala wa sheria, haki za binadamu na uhuru wa msingi katika kipindi chote cha uchaguzi”.

Umuhimu wa uchaguzi huu

Taarifa hiyo pia imebainisha umuhimu wa uchaguzi wa manispaa, ambao haujafanyika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwaka 1988.

Katibu Mkuu amesema kufanyika kwa uchaguzi huo ni hatua ya kihistoria katika mchakato wa amani na ameielezea kama “hatua muhimu kuelekea kuimarisha ugatuzi wa mamlaka ya dola,” kama ilivyobainishwa katika Mkataba wa Kisiasa wa Amani na Maridhiano wa mwaka 2019.

Guterres pia ametambua mchango wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Amani nchini humo, MINUSCA, akibainisha msaada wake unaoendelea kwa mamlaka za kitaifa katika kuandaa na kusimamia uchaguzi huo, kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP.

Heko kwa maandalizi ya uchaguzi

Aidha, Katibu Mkuu amezipongeza juhudi za mamlaka za Jamhuri ya Afrika ya Kati na wahusika wote waliotoa mchango katika maandalizi ya uchaguzi huo, akisisitiza tena dhamira ya Umoja wa Mataifa kuendelea kuunga mkono nchi hiyo.

Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati katika juhudi zake za “kuimari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *