Milipuko mikubwa iliyoambatana na sauti zinazofanana na ndege zinazoruka juu ya ardhi imesikika yapata saa 2:00 asubuhi (7:00 asubuhi saa za Ufaransa) leo Jumamosi huko Caracas, mwandishi wa habari wa AFP ameripoti. Katika vitongoji vingi, wakazi wamekimbilia kwenye madirisha ya nyumba zao kujaribu kuelewa kinachoendelea.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Picha za moto mkubwa wenye moshi mwingi zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii, lakini haiwezekani kubainisha eneo halisi la milipuko hiyo, ambayo inaonekana kutokea kusini na mashariki mwa mji mkuu wa Venezuela. Milipuko imeendelea kusikika yapata saa 8:15 asubuhi (7:15 asubuhi saa za Ufaransa).

Milipuko pia imesikika katika uwanja wa ndege na bandari ya Caracas, mkazi wa La Guaira ameliambia shirka la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina. Wakazi wengine wameliambia shirika hili la habari la Ufaransa kwamba walisikia milipuko huko Higuerote, yapata kilomita 100 (maili 60) mashariki mwa Caracas. Katika vitongoji vingi, wakazi wamekimbilia kwenye madirisha na ya nyumba zao kujaribu kuelewa kinachoendelea. Umeme umekatika katika baadhi ya maeneo ya jiji, kulingana na wakazi.

Milipuko hiyo, ambayo baadhi yake imetikisa madirisha kutoka maili kadhaa na maeneo husika, ilifanya iwe vigumu kubaini mara moja mahali halisi panakoripotiwa milipuko hiyo. Inaonekana kutokea kusini na mashariki mwa mji mkuu wa Venezuela, na labda huko Fuerte Tiuna, eneo kubwa la kijeshi ndani ya jiji.

Milipuko hii inakuja huku Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ametuma meli ya majini kwenda Karibiani, akiongeza uwezekano wa mashambulizi ya ardhini dhidi ya Venezuela na kusema kwamba siku za Rais wa Venezuela Nicolas Maduro “zinahesabiwa.”

Siku ya Jumatatu alitangaza kwamba Marekani iliharibu eneo la kuegesha meli linalotumiwa na meli zinazoshutumiwa kushiriki katika biashara ya dawa za kulevya nchini Venezuela, katika kile ambacho kingekuwa shambulio la kwanza la ardhini la Marekani kwenye ardhi ya Venezuela.

Rais Maduro, kwa upande wake, alionyesha imani katika mahojiano yaliyoruwa siku ya Alhamisi, akisema: “Mfumo wa ulinzi wa taifa umehakikisha na unaendelea kuhakikisha uadilifu wa eneo, amani ya nchi, na matumizi na starehe ya maeneo yetu yote.”

Donald Trump anamtuhumu rais Maduro kwa kuongoza mtandao mkubwa wa biashara ya dawa za kulevya, jambo ambalo Maduro anakanusha, akiishutumu Marekani kwa kutaka kumpindua ili kunyakua akiba ya mafuta ya nchi hiyo, ambayo ni kubwa zaidi duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *