Chombo cha diplomasia cha Iran kimesisitiza kuwa imesisitiza katika taarifa yake kwamba: Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani vikali mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela na ukiukaji mkubwa wa mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela na kuikuka pakubwa mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya nchi hiyo. 

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema: Mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela ni ukiukwaji wa wazi wa kanuni za msingi za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kanuni za msingi za sheria za kimataifa, hasa kifungu cha 2, aya ya 4, ya Mkataba huo, ambayo inakataza matumizi ya nguvu, na ni mfano kamili wa “hujuma ya kichokozi” ambayo inapaswa kulaaniwa waziwazi haraka iwezekanavyo na bila shaka  na Umoja wa Mataifa na serikali zote zinazohusika na uheshimishwaji wa utawala wa sheria, amani na usalama wa kimataifa.

Uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya nchi huru ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa ni ukiukaji mkubwa wa amani ya kikanda na kimataifa, ambayo matokeo yake yataathiri mfumo mzima wa kimataifa na kuutia katika hatari kubwa ya kusambaratika na kuharibika mfumo huo unafuata Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sanjari na kukumbusha juu ya haki ya asili ya Venezuela ya kutetea mamlaka yake ya kitaifa, umoja wa ardhi na haki yake ya kujitawala, imesisitiza juu ya kuwajibika kisheria na kimaadili  serikali zote na mashirika ya kimataifa hususan Umoja wa Mataifa na Baraza lake la Usalama ili kusimamisha haraka iwezekanavyo hujuma haramu ya Marekani dhidi ya Venezuela; na kusisitiza juu ya haja ya kuchukuliwa hatua zinazohitajika na za lazima ili kuwawajibisha wapangaji na wahusika wa uvamizi huo wa kijeshi dhidi ya Venezuela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *