
Afrika Kusini imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha kikao cha dharura kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela, na kukamatwa Rais wa nchi hiyo Nicholas Maduro na mkewe.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imeeelzea kuwa: ” Utumiaji nguvu usio halali, wa upande mmoja kama huo unadhoofisha uthabiti wa utaratibu wa kimataifa na kanuni ya usawa miongoni mwa mataifa.”
Serikali ya Pretoria imeeleza kuwa ina wasiwasi mkubwa na matukio ya Venezuela na kwamba hatua za Marekani dhidi ya nchi hiyo ni ukiukaji wa wazi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambao unaziamuru nchi zote wanachama kujiepusha na vitisho au matumizi ya nguvu dhidi ya mamlaka ya kujitawala na uhuru wa kisiasa wa nchi yoyote.
Taarifa ya serikali ya Afrika Kusini imeongeza kuwa: Mkataba hauidhinishi uingiliaji wa kijeshi wowote wa nchi ajinabi masuala ambayo kimsingi yako ndani ya mamlaka ya ndani ya nchi huru.
Ras Donald Trump wa Marekani mapema jana alisema kuwa Washington imefanya mashambulizi makubwa dhidi ya Venezuela na kwamba Maduro na mke wake Cicila Flores wamekamatwa na kusafirishwa nje ya nchi. Trump amesema mashambuliz hayo yametekelezwa
Baada ya kukamatwa Rais wa Venezuela na mkewe, baadaye Rais wa Marekani aliiambia televisheni ya Fox News kwamba Washington inaweza kuwa na jukumu la moja kwa moja katika kuunda mustakabali wa Venezuela kufuatia kuondolewa Maduro.