
VIKAO vya Kamati za Kudumu za Bunge vinatarajiwa kuanza Januari 13 hadi 23, 2026 jijini Dodoma.
Taarifa ya Bunge imesema vikao hivyo ni kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Bunge unaotarajiwa kuanza Januari 27, 2026.
Imesema shughuli zilizopangwa kutekelezwa na kamati hizo ni pamoja na uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, kamati kuzifahamu wizara na taasisi zote na baadhi ya sera na sheria kulingana na majukumu ya kila kamati, kamati kupitishwa kwenye majukumu yake ya msingi na kamati ya bajeti kufanya maandalizi ya hoja zitakazojadiliwa na Bunge.