Angalau watu wanne wameuawa leo Jumatano, Januari 7, kusini magharibi mwa Yemen, kulingana na vyanzo vya hospitali. Zaidi ya mashambulizi 15 ya anga ya Saudi Arabia yamelenga jimbo la kiongozi wa waasi aliye mafichoni, Aidarous al-Zoubaidi,  kusini magharibi mwa Yemen, afisa wa eneo hilo ameripoti.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya katika jimbo la Dhale (kusini magharibi) yamelenga viongozi waaminifu kwa Aidarous al-Zoubaidi, chanzo hicho kimeliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina. Aidarous al-Zoubaidi, ambaye anaongoza Baraza la Mpito la Kusini (STC), ambalo linatafuta kuanzisha jimbo kusini mwa Yemen, ametangazwa kuwa mafichoni siku ya Jumatano, wakati alitarajiwa kusafiri kwenda Riyadh kwa mkutano uliokusudiwa kuleta amani kati ya makundi mbalimbali yanayowania udhibiti wa nchi.

Yemen: Kiongozi wa waasi Aidarous al-Zoubaidi afukuzwa kutoka Baraza la Rais kwa “usaliti mkubwa”

Kiongozi wa waasi wa kusini mwa Yemen, Aidarous al-Zoubaidi, amefukuzwa kutoka Baraza la Rais kwa “usaliti mkubwa,” mkuu wa chombo hiki kinachoongoza serikali kinachotambuliwa kimataifa ametangaza leo Jumatano, Januari 7. Aidarous al-Zoubaidi atafikishwa “mbele ya Mwanasheria Mkuu,” ofisi ya rais imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari, ikimtuhumu kwa mfululizo wa uhalifu.

Waasi wa kusini mwa Yemen wanaungwa mkono na Falme za Kiarabu na wanashutumiwa na Saudi Arabia kwa kutishia usalama wa kikanda. Lengo lililotajwa la wanaotaka kujitenga ni kurejesha taifa huru kusini mwa Yemen, katika eneo la Jamhuri ya zamani ya Kidemokrasia ya Watu wa Yemen, ambayo ilikuwepo kati ya mwaka 1967 na 1990.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *