Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2025 imeingia hatua ya robo fainali.

Hii ni baada ya hatua ya makundi na mtoano kuibua matokeo ya kushangaza, na sasa macho ya mashabiki yameelekezwa kwenye mechi nne za kusisimua zitakazochezwa mwishoni mwa wiki hii.

Ijumaa hii, timu ya taifa ya Mali itachuana na miamba Senegal katika mchezo unaotajwa na wachambuzi kama mmoja wa michezo migumu zaidi katika hatua ya robo fainali wakati Cameroon wakiingia uwanjani siku hiyo hiyo kuvaana na wenyeji Morocco.

Morocco inatumai kutumia faida ya kucheza nyumbani na ubora wa kikosi chenye wachezaji waliotamba kwenye Kombe la Dunia 2022.

Alafu siku ya Jumamosi, itakuwa ni zamu ya Algeria, mabingwa wa AFCON mwaka 2019 kupambana na Super Eagles Nigeria kabla ya Misri kumaliza udhia na mabingwa watetezi Ivory Coast.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *