
Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, ameagiza kuanzishwa kwa msako wa wanamgambo walioshambulia soko katika jimbo la Niger, mashambulizi yaliyosababisha vifo vya takriban watu 50 katika mojawapo ya mashambulio mabaya zaidi ya hivi karibuni katika eneo hilo.
Shambulio lilitokea katika soko la Kasuwan Daji katika kijiji cha Demo, ambapo wanamgambo waliokuwa na silaha walivamia eneo hilo Jumamosi, wakipiga risasi ovyo, kuwateka nyara wakazi na kuiba vyakula, kulingana na taarifa za eneo hilo. Mazishi ya pamoja yamefanywa kwa wahanga, huku waliojeruhiwa wakiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali za karibu.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X Jumapili, Rais Tinubu alilaani ghasia hizo na kuagiza viongozi wa usalama kuwatafuta wahusika.
“Nimewaamuru Waziri wa Ulinzi, Mkuu wa Maafisa wa Ulinzi, Wakuu wa Idara za Huduma za Kijeshi, Kamishna Mkuu wa Polisi, na Mkurugenzi Mkuu wa DSS kuwatafuta magaidi waliosababisha shambulio la Kasuwan Daji na kuhakikisha wanafikishwa haraka mbele ya sheria,” alisema.
“Magaidi hawa wamejaribu azma ya nchi yetu na watu wake. Lazima wawajibishwe kwa kikamilifu kwa vitendo vyao vya uhalifu,” aliongeza rais. “Haijalishi ni nani au nia yao ni ipi, lazima watafutwe. Wale wanaowaunga mkono, kuwasaidia au kuwawezesha pia watafikishwa mbele ya sheria.”
‘Linda jamii zilizo hatarini’