Katika mkakati wa kuhakikisha wazazi wanaolea watoto wenye Usonji au Autism wanalea watoto wao bila kubaguliwa shuleni ,kwenye jamii au kukosa nafasi bora za elimu,shule maalum ya Mali jijini Nairobi imeanzisha mpango ambapo wanafunzi wanasoma ,kutunzwa na maslahi ya wazazi wao yakishughulikiwa pia.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa wazazi wengi nchini Kenya ,kumlea mtoto mwenye usonji ,Autism ,si malezi ya kawaida,ni malezi yenye mzigo mzito ,gharama  na inanyanyapaisha .

Carol Korir ametupeleka kwenye shule ya jumuishi ya Mali eneo la Karen jijini Nairobi kuelewa namna ambavyo watoto hao maalum wanaweza kujifunza ,kukuza vipaji vyao na wazazi wao kurahisishiwa mzigo wa ulezi.

Kwa wazazi na walezi wa watoto hao,Siku zao hutumika kwenye ziara za kliniki za kutoa tiba  nasaha  ambazo huwa ghali  na kujaa unyanyapaa kutoka kwa jamii. 

Kwenye   Mali Integrated School  , ambayo itakuwa ya kwanza  Afrika Mashariki  mambo ni tofauti kidogo.

Hapa wanafunzi watapata masomo yanayoendana na mahitaji yao ,walimu wakitumia mbinu bunifu kama muziki kuwapa elimu.

Hao ni walimu wa muziki wanaowahudumia watoto hao.

“ Wewe unamchezea tu jambo moja halafu anarudia kwa kukumbuka ,” alisema mmoja wa walimu.

“ Unahakikisha uko naye hapo kisha unamwonesha hii namna ya kushika,” alielezea mwalimu pia

“Wengi wao tukiwachezea muziki wanatulia,” alisema mwalimu mwingine.

Mwasisi wa Shule hii Elizabeth Pauline Wamukowa ,anasema kilichomchea ni mtoto wake Daniel Mali  ambaye ana usonji, na  sasa masomo yake yako hatarini kwa kuwa hamna shule inayomfaa.

“Mimi hupenda kutumia mtoto wangu kama Compass kwa mfano saa hii  amefanya mtihani wa Gredi 6,wenzake wanaendelea na Gredi 7 lakini yeye amekaaa nyumbani,sababu shule ile yupo haiwezi kushughulikia mahitaji yake  kabisa ya kimasomo,”alielezea Elizabeth Pauline Wamukowa.

Shule hii maalum pia inazingatia wazazi na walezi ,mahali ambapo wanaweza  kupumzikia  wanao pia wakishugulikiwa.

Hao ni baadhi kwa wazazi hao.

“ Tunahitaji hata sehemu ya kulala kwa sababu wakati mwingine watoto wetu hawalali,” alisema mzazi mmoja.

“ Sitahangaika kutafuta shule,” alisema mzazi mwingine kwa Jina Vanessa.

Shirika la afya duniani ,limebaini ongezeko la watu wenye usonji Ongezeko hili likimanisha  uhitaji mkubwa wa matunzo maalum, na shule ya Mali ni moja ya ufumbuzi unaolenga kutatua changamoto hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *