#HABARI: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Kinondoni, imefanikiwa kuwakamata raia wawili wa China, Yao Licong na Wang Weisi, wakiwa na kiasi kikubwa cha fedha haramu kinachozidi Shilingi Bilioni 2.
Watuhumiwa hao, ambao ni wakazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, walinaswa Januari 5, 2026, wakiwa na Dola za Kimarekani 707,075 pamoja na fedha za Kitanzania zilizohifadhiwa kwenye mifuko ya sandarusi ndani ya gari lao.

Ukamataji huo ni matokeo ya operesheni maalum iliyodumu kwa miezi saba kuanzia Mei 2025, ikishirikisha Benki Kuu (BoT), TRA, na mabenki mengine kuchunguza mtandao wa uhalifu wa kadi za benki.

Inashukiwa kuwa fedha hizo ni mazalia ya utakatishaji wa fedha uliotokana na wizi wa taarifa za kadi za benki (stolen card details) za raia wa nje, ambapo fedha huchotwa kwenye akaunti zao na kuonekana zimetumika kulipia huduma nchini Tanzania kinyume cha sheria.

Watuhumiwa hao wameshindwa kuthibitisha uhalali wa fedha hizo kwa kukosa biashara rasmi au stakabadhi za kubadilishia fedha za kigeni walizokutwa nazo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TAKUKURU leo Januari 7, 2026, uchunguzi bado unaendelea ili kuwakamata washiriki wengine wa mtandao huo, huku watuhumiwa waliokamatwa tayari wakiwa wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *