‎#HABARI: Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Mbeya walionusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Bahari Beach (T997 EHP) kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso (T283 EEB) katika eneo la Chamakweza, Chalinze mkoani Pwani, wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo, ambaye alikuwa akiendesha kwa mwendokasi mkubwa tangu walipoanza safari yao.

Kufuatia ajali hiyo, wananchi na abiria hao wameiomba Serikali kupitia Jeshi la Polisi kuchukua hatua madhubuti za kuwadhibiti madereva wazembe na kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinasimamiwa kikamilifu ili kupunguza vifo na majeruhi nchini.

Wakati huohuo, jitihada za waandishi wa habari kupata taarifa rasmi na za kina kutoka kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kuhusu idadi kamili ya majeruhi au vifo zimeendelea.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *