Wanajeshi wa Ujerumani wamekuwa wakipangiwa jukumu nchini Poland kwa miaka mingi kama sehemu ya misheni mbalimbali za Umoja wa Kujihami NATO, na kuongeza kuwa uwepo wa wanajeshi wao katika ardhi ya Poland lisingekuwa jambo jipya.

Sikorski alikuwa akizungumza baada ya mashauriano mjini Paris na mawaziri wenzake wa Ufaransa na Ujerumani, Jean-Noël Barrot na Johann Wadephul, katika kile kinachoitwa muungano wa ushirikiano wa pande tatu wa Weimar.

Ujerumani na Poland zipo vyema katika ushirikiano wa kijeshi

Alibainisha kuwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Poland na Ujerumani tayari umeimarika. Wakati wa mazoezi ya pamoja miaka kadhaa iliyopita, jenerali wa Kijerumani aliiongoza brigadi ya mizinga ya Poland, huku jenerali wa Kipoland akiiongoza brigadi ya Kijerumani.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Poland pia aliishukuru Ujerumani kwa hatua ya mwaka jana ya kupeleka wanajeshi kusaidia kuulinda uwanja wa ndege karibu na Rzeszow, kusini mashariki mwa Poland, kituo muhimu kwa msaada wa kijeshi na kibinadamu kwa Ukraine.

Ujerumani 2025 | Mwanajeshi wa jeshi la Ujerumani wakati wa mazoezi ya kijeshi
Ujerumani 2025 | Mwanajeshi wa jeshi la Ujerumani wakati wa mazoezi ya kijeshiPicha: Joeran Steinsiek/STEINSIEK.CH/IMAGO

Itakumbuka Jumanne, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz kwa mara ya kwanza alionesha uwezekano wa jeshi la Ujerumani kushiriki katika operesheni za kulinda amani ikiwa si ndani ya Ukraine, bali katika eneo la NATO karibu na mpaka.

Sikorski akisema kuwa iwapo usitishaji wa mapigano utapatikana na operesheni ya kulinda amani kuanzishwa nchi kadhaa ikiwa pamoja na Ufaransa kama taifa kiongozi tayari zimekubaliana kuhusu hatua za maandalizi nchini Poland. Aliongeza kuwa mipango ya kina hatimaye itashughulikiwa na makao makuu ya kijeshi ya nchi husika.

Serikali ya Ujerumani ilisema mazungumzo mjini Paris yalilenga kuendeleza dhamana thabiti za usalama kwa Ukraine baada ya usitishaji wa mapigano na mchango wa Ulaya katika usalama wa muda mrefu. Muungano wa ushirikiano wa pande tatu wa Weimar ulianzishwa mwaka 1991 kama jukwaa la mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa wakati huo wa Ujerumani, Ufaransa na Poland.

Mashambulizi ya Urusi yaua watu wawili nchini Ukraine

Ndani nchini Ukraine, Watu wawili wameuawa na wengine wanane kujeruhiwa katika shambulio la Urusi kwenye bandari karibu na jiji la Odessa lililo kando ya Bahari Nyeusi.

Kupitia ukurasa wake wa Telegram, Gavana wa mkoa wa Odessa, Oleh Kiper ameandika pamoja na mauwaji hayo yalisababisha uharibifu wa miundombinu katika bandari za Pivdennyi na Chornomorsk akisambaza picha zinazoonyesha makontena ya mizigo yaliyoharibiwa na malori yaliyopata madhara.

Vyombo vya habari vya Ukraine viliripoti kuwa milipuko pia ilisikiwa katika jiji la Odessa lenyewe. Bandari za Bahari Nyeusi ni muhimu kwa mauzo ya nje ya nafaka na bidhaa nyingine za kilimo za Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *