Akizungumza na waandishi habari mjini Roma, Meloni amesema anadhani wakati umefika kwa Ulaya kuzungumza na Urusi, kwa sababu ikiwa Ulaya itaamua kushiriki katika awamu hii ya mazungumzo yanayoendelea, kuzungumza na upande mmoja kati ya pande zinazohusika, mchango chanya ambao inaweza kutoa ni mdogo.

Meloni amesema ni vigumu kujua ni nani upande wa Umoja wa Ulaya atakayeshiriki katika mazungumzo hayo.

Meloni pia amesema amekuwa akiunga mkono kuteua mjumbe maalum wa Ulaya kuhusu suala la Ukraine, ambaye angefuatilia na kuwashauri ili kuwaruhusu kuzungumza kwa sauti moja.

Hata hivyo, amesema ni mapema mno kuzungumzia kuikaribisha tena Urusi katika kile ambacho kwa sasa ni kundi la nchi saba zilizostawi kiviwanda za G7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *