#HABARI: Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Zainab Katimba ameeleza kuwa ukatili wa kijinsia ni kosa la jinai na kila mwanachi wa Tanzania ana haki na wajibu wa kuripoti matukio hayo ili kuhakikisha waathirika wanapatiwa ulinzi na haki inatendeka

Mhe. Katimba amesema hayo mkoani Singida wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Huduma za Msaada wa Kisheria uliofanywa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera.

Ameeleza kuwa matukio ya ukatili yanaweza kuripotiwa katika vituo vya Polisi, kupitia dawati la jinsia na watoto katika ofisi za Ustawi wa Jamii, vituo vya afya au hospitali na kupitia madawati ya watoa huduma za msaada wa kisheria yaliyopo katika kila halmashauri

“Serikali imeweka namba maalumu ya bure ya kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto ambayo ni 116, na namba ya Wizara kupitia kituo cha huduma kwa mteja 0262160360.” Amesema Mhe. Katimba

Vilevile amefafanua kuwa Ukatili wa Kijinsia ni kitendo au vitendo vya unyanyasaji au mateso anavyofanyiwa mtu kwa misingi ya jinsia yake na kusababisha madhara ya kimwili, Kihisia, Kisaikolojia au Kiuchumi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *