‎#HABARI: Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, amefunga rasmi kikao cha tathmini ya utendaji kazi kwa nusu mwaka wa fedha 2025/2026, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji, ubunifu na utoaji wa huduma bora kwa walipakodi ili kuongeza mapato ya Taifa.

‎Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Bw. Mwenda amesema mafanikio ya ukusanyaji wa mapato yanatokana na jitihada za pamoja za watumishi wa TRA katika kuimarisha mifumo ya usimamizi, matumizi ya teknolojia na utoaji wa huduma rafiki kwa walipakodi.

‎Amesema kuwa ni wajibu wa kila mtumishi wa Mamlaka hiyo kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa uadilifu, ubunifu na kwa kuzingatia thamani ya fedha za umma ili kufikia malengo ya Serikali katika ukusanyaji wa mapato.

‎Aidha, Bw. Mwenda amewataka watumishi wa TRA kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi, kuwasikiliza walipakodi na kutatua changamoto zao kwa wakati ili kuongeza uaminifu na utayari wa kulipa kodi kwa hiari.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *