Pezeshkian amewataka raia wa Iran kujitenga kabisa na wale alowataja kuwa “wahalifu na magaidi kwa taifa hilo.”

Hayo yanajiri wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisema anatumai hivi karibuni Iran itajinasua kutoka “mikononi mwa udhalimu” huku maandamano hayo makubwa yakiendelea kusambaa kote nchini humo.

Amesema hilo likifanyika Iran na Israel zitarejea kuwa “washirika wa kweli na kujenga siku za usoni zilizo na ustawi na amani kwa watu wa mataifa yote mawili.”

Nayo Uingereza kwa upande wake imesema ingependa kuona mabadilishano ya amani ya madaraka nchini Iran mnamo siku za usoni.

Waziri wa uchukuzi Heidi Alexander amesema Uingereza siku zote inaiona serikali mjini Tehran kuwa kitisho kwa amani ya mashariki ya kati na imekuwa ikiwakandamiza raia wake.

Waandamanaji nchini Iran wamekuwa wakipinga kile wanachokitaja kuwa sera mbovu za serikali ambazo wanadai zimechangia kuanguka kwa uchumi wa taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *