Katika taarifa yake iliyotolewa hii leo jumapili Januari 11, 2026 jijini New York Marekani na Msemaji wake Stéphane Dujarric ameeleza kuwa Wairani wote lazima waweze kuelezea malalamiko yao kwa amani na bila woga. 

“Haki za uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukusanyika kwa amani, kama ilivyoainishwa katika sheria za kimataifa, lazima ziheshimiwe na kulindwa kikamilifu.” Imesema taarifa hiyo.

Katibu Mkuu anazisihi mamlaka za Iran “kujizuia kabisa na kujiepusha na matumizi yasiyo ya lazima au yasiyo ya usawa ya nguvu.”

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameendelea kuhimiza hatua zinapaswa kuchukuliwa ambazo zinawezesha upatikanaji wa taarifa nchini humo, ikiwa ni pamoja na kurejesha mawasiliano.

Taarifa zinaeleza kuwa huduma ya mawasiliano ya intaneti imefungwa nchini humo kufuatia maandamano yanayoendelea katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo. 

Hapo jana ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa Kuchunguza Ukweli kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulitoa taarifa wakiitaka serikali ya Iran kurejesha mara moja huduma za intaneti na mawasiliano ya simu, pamoja na kusitisha ukandamizaji wa kikatili dhidi ya maandamano yanayoendelea nchi nzima.

Soma zaidi kuhusu taarifa hiyo hapa. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *