
Boti iliyokuwa imebeba watu 300 kutoka nchi za Afrika Magharibi, ambayo iliondoka pwani ya Gambia zaidi ya mwezi uliyopita, haijulikani ilipo. Boti hiyo, iliyokuwa ikielekea Uhispania, iliondoka katika mji wa Djinack nchini Gambia mnamo Desemba 5 yapata saa 1 usiku. Katika siku za hivi karibuni, watu kadhaa wadau katika masuala ya uhamiaji nchini Senegal walionya. Wana hofu kuwa huenda boti hiyo ilizama baharini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Dakar, Pauline Le Troquier
Boti hiyo ilionekana mara ya mwisho katika pwani ya Joal nchini Senegal, siku moja baada ya kuondoka kwake kutoka Gambia, mnamo Desemba 6. Katika video iliyorekodiwa na mvuvi siku hiyo, boti hiyo iliyojaa watu wengi inaonekana ikijitahidi kusonga mbele katika mazingira magumu ya upepo na mawimbi makubwa baharini . Ndani ya boti hiyo walikuwa wahamiaji vijana kutoka Senegal, Gambia, Mali, na Guinea.
Mamadou Mignane Diouff ni mratibu wa Jukwaa la Kijamii la Senegal anatoa wito kwa mamlaka kuanzisha utafutaji wa kina wa watu wanaoshukiwa kutoweka. “Safari kwa kawaida huchukua wiki moja, siku kumi. Tuna maswali kwa sababu tunaamini kwamba leo, kuna uwezo wa kutosha, rada, ndege, na meli zilizotumwa kuzuia, au angalau kupata, boti zilizo katika htari ya kuzama.”
Kadri udhibiti umekuwa mgumu huko Dakar, waaosafiri kuelekea Ulaya wamehamia kusini zaidi kuelekea Gambia na Visiwa vya Saloum. Matokeo yake, muda wa kuvuka ni mrefu zaidi na hatari ya boti kuzama inaongezeka. Saliou Diouf ni kiongozi wa shirika la Boza Fii kutoka nchini Senegal, ambalo linatetea haki za wahamiaji. Analaani hasa ukosefu wa rasilimali za uokoaji. “Kwa bahati mbaya, hakuna meli za kibinadamu katika Atlantiki. Kilicho hakika ni kwamba ukandamizaji ndio unaofanya mambo kuwa hatari zaidi. Mifumo ya ufuatiliaji haipo ili kuwaokoa watu. Ipo tu ili kuwaacha watu wafe baharini.”
Kila mwaka, maelfu ya wahamiaji huondoka kutoka pwani ya Morocco ya Afrika Magharibi, wakijaribu kufika Visiwa vya Canary kwa njia ya baharini. Mnamo mwaka 2025, zaidi ya watu 1,900 walikufa maji wakati wakivuka bahari, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Caminando Fronteras.