
Shambulio la Urusi katika mji wa Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine limewaua watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Taarifa hiyo imetolewa mapema leo na gavana wa mkoa Oleg Synegubov akisema kufikia sasa, watu wawili wanajulikana kuuawa na mashambulizi ya adui nje kidogo ya Kharkiv, akiandika kwenye mtandao wa Telegram.
Pia alisema watu wengine watatu walijeruhiwa katika shambulio hilo la usiku kucha.
Urusi imeishambulia Ukraine kwa ndege zisizo na rubani na makombora ya kila siku katika miezi ya hivi karibuni, ikilenga miundombinu ya nishati na kukatisha umeme katika kilele cha baridi kali.