Ukitambuliwa rasmi kama BMkataba wa Kimatafa wa Hifadhi ya Bayonuia kwenye maeneo ya maji ya bahari yaliyo nje ya usimamizi wa kitaifa, au BBNJ mkataba huu wenye nguvu kisheria unahusisha maeneo ya Bahari yaliyo nje ya usimamizi wa taifa moja moja halikadhalika sakafu ya bahari. 

Tazama video ya mahojiano ya Assumpta Massoi na Mtaalamu kutoka Tanzaina kuhusu faida za BBNJ

Maeneo hayo yanachukua zaidi ya theluthi mbili ya uso wa eneo la uso wa Bahari, ikiwa ni zaidi ya asilimia 90 ya ujazo wa eneo la makazi la dunia. Hii ni kwa sababu baharí ina kina kirefu, na eneo kubwa la dunia liko chini ya maji.

Haya ni mambo muhimu ya kufahamu kuhusu BBNJ

Kwa nini ni muhimu

Mkataba huu BBNJ umeandaliwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye ‘Bahari Kuu’ na eneo la kimataifa la sakafu ya Bahari ili yawe ni mazingira ambayo yanatumika na kusimamiwa kwa uendelevu kwa maslahi ya binadamu wote.

Halikadhalika ni mkataba wa kwanza wenye nguvu kisheria kuhusu Bahari ambao unapatia jukumu la pamoja la usimamizi, kukiwa na vipengele kuhusu watu wa jamii ya asili bila kusahau usawa wa kijinsia.

Uhai mbalimbali wa baharini unatarajiwa kulindwa vizuri zaidi kutokana na mkataba mpya.

© The Ocean Story/Vincent Kneefel

Viumbe hai mbalimbali vya baharini unatarajiwa kulindwa vizuri zaidi kutokana na mkataba mpya.

Ni matumaini kwamba pindi utakapotekelezwa kwa ukamilifu wake, Mkataba huu utakuwa na mchango muhimu katika kutatua kile kinachoitwa “janga la utatu la sayari” ambalo ni mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa bayonuai na uchafuzi.

Akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Mzee Ali Haji ambaye aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye majadiliano ya BBNJ amesema mkataba huu ni hatua muhimu sana katika kulinda eneo la Bahari Kuu.

Kila mtu anapaswa kutambua kuwa kwa sasa kuna udhibiti wa kinachofanyika kwenye Bahari kuu. Mathalani unapofanya uchafuzi, badi utawajibika kwa matendo yako.”.

Mkataba huu unaimarisha mfumo wa sasa ulioko wa kimataifa wa udhibiti: unaendeleza Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sheria ya Bahari (UNCLOS) – ujulikanao kama “Katiba ya Bahari” – ambao umeweka kanuni za baharini na utoaji wa rasilimali za sakafu ya Bahari na ulinzi wa viumbe vya habarini. Mkataba huo ulianza kutumika mwaka 1994.

Mkataba wa sasa unaziba mapengo yaliyomo kwenye UNCLOS, ikiwemo hatua za kina ya jinsi ya kusimamia bayonuai na kuweka usimamizi wa Bahari wakati huu kuna changamoto mpya kama mabadiliko ya tabianchi na Ajenda ya 2030 kuhusu Malengo y aMaendeleo Endelevu 

Kuanza kutumika kwa mkataba kuna maana gani?

Baada ya mkataba kuanza kutumia, unakuwa na nguvu kisheria kwa mataifa 81 ambayo hadi sasa yameridhia. Ina maana kwamba wamekubali kujumuisha mkataba huo katika sheria zao za kitaifa au za nchi.

Mkataba unaainisha kuwa utaanza kutumia Jumamisi hii: siku 120 baada ya kuridhiwa – au kukubaliwa kisheria na angalatu nchi 60.

Nani amesaini na nani hajatia Saini?

Nchi zenye uchumi mkubwa ambazo zimesaini na kuridhia BBNJ ni China, Ujerumani, Japan, Ufaransa na Brazil

China ina umuhimu mkubwa kwenye viwanda vinavyohusiana na Bahari, kama vile (ujenzi wa meli, ufugaji Samaki, uvuvi, na uchimbaji wa mafuta na gesi baharini). Mwaka 2023 iliuza bidhaa zihusianazo na bahari zenye thamani ya thamani ya dola bilioni 155, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCATD. 

Ambao hawaridhia ni Marekani, India, Uingereza na Urusi

Marekani, ambayo inaongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa zaidi duniani, ni moja ya nchi 5 zinazoongoza kwa kuuza nje ya nchi bidhaa zitokazo kwenye baharí. (Dola bilioni 61) INgawa ilitia Saini mkataba huo mwaka 2023, bado haijaridhia, na Baraza la Seneti halijachukua hatua yoyote ile.

India nayo, moja ya nchi zinazoendelea zenye uchumi mkubwa na zinazoongoza kwa kuuza nje ya nchi bidhaa, (dola bilioni 19) iliridhia mkataba mwaka 2024, lakini bado kuridhia. Uingereza nayo ilianzisha mchakato wa sheria ya ndani mwaka 2025, lakini bunge bado halijaridhia.

Urusi, inasalia moja ya nchi chache ambazo hazijatia saini wala kuridhia, BBNJ, ikieleza kuwa inataka kuendeleza mifumo ya sasa ya usimamizi wa Bahari kuu , na kuhakikisha kuna uhuru wa kupita maeneo ya kimataifa baharini.

Je hiki ni kikwazo kikubwa kwa BBNJ?

Licha ya baadhi ya mataifa makubwa kusita sita kutia saini na kuridhia mkataba huu, Bwana Haji bado ana matumaini kuwa BBNJ utakuwa na manufaa katika hali ya sasa ilivyo.

“Nchi zinazoendelea na nchi za visiwa vidogo wanahitaji msada,” amesema. “Tunatarajia kuwa katika siku zijazo, nchi zinazositasita zitakuwa mkataba huu, kwa sababu utawasaidia. Ulinzi wa eneo la bahari kuu ni wajibu wetu sote.”

Nini kinafuata?

Mlango uko wazi kwa nchi kuridhia, hatua ambayo itafanya mkataba kuwa fanisi zaidi.

“Unapofanya majadiliano na mashauriano ya kitu Fulani, huwezi kupata asilimia 100 ya watu wote kuridhia au kukubali kwa wakati mmoja,” amesema Bwana Haji, “Baadhi wanatazama tu, na kicha wakianza kuona manufaa yake watajiunga. Ninaamini kuwa katika siku zijazo wengine watajiunga.”

Mbali na ushiriki wa wote, jambo muhimu la kuhakikisha kuwa BBNJ inafanya kazi litakuwa ni utekelezaji—yaani, kuchukua hatua dhidi ya wale wanaokiuka sheria.
Kulingana na yaliyomo kwenye mkataba, mkutano wa kwanza wa kufuatilia maendeleo katika maeneo yote mawili utafanyika si zaidi ya mwaka mmoja baada ya mkataba huu kuanza kutumika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *