#HABARI: Wizara ya Katiba na Sheria, kupitia kliniki yake ya msaada wa kisheria, imefanikiwa kumfikia Mzee Jumanne Ngaiza, mkazi wa mtaa wa Unyankahe mkoani Singida, ili kutatua mgogoro wa ardhi uliomsumbua kwa muda mrefu. Huduma hii ni sehemu ya mikakati ya wizara kuendelea kugusa maisha ya Watanzania wenye kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za mawakili. Mzee Ngaiza alipata fursa ya kipekee ya kuwasilisha malalamiko yake moja kwa moja kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, wakati wa kliniki hiyo iliyofanyika Januari 9, 2026.

Baada ya kusikilizwa kwa hoja hizo, timu ya wataalamu kutoka wizarani na Manispaa ya Singida, kwa kushirikiana na ofisi ya mtaa, walifanya ziara ya haraka hadi kwenye eneo la mgogoro ili kujiridhisha na uhalisia wa malalamiko yaliyowasilishwa. Hatua hii ya kufika ‘site’ ililenga kupata suluhu ya kudumu na ya haki kwa Mzee Jumanne, ikionyesha dhamira ya dhati ya serikali katika kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mwananchi bila kujali hali yake ya kiuchumi.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *