‎#HABARI: Jopo la Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ujerumani (German Agribusiness Alliance) limeahidi kushiriki katika Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa ya Wakulima – Nane Nane 2026, yanayotarajiwa kufanyika nchini Tanzania kuanzia Agosti 1 hadi 8, 2026.

‎Ahadi hiyo imetolewa wakati wa Mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Tanzania na Ujerumani (Tanzania Business/Investment Roundtable Meeting) ulioongozwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo, pembezoni mwa Jukwaa la Kimataifa la Chakula na Kilimo (GFFA) linalofanyika nchini Ujerumani.

‎Katika mkutano huo, Tanzania iliwasilisha fursa mbalimbali za uwekezaji katika Sekta ya Kilimo zikiwemo kukuza uzalishaji na uchakataji wa mazao ya mbegu za mafuta (alizeti na chikichi), ngano na soya, kupanua biashara ya kokoa, kahawa na korosho, kuendeleza uwekezaji katika miundombinu ya uhifadhi, usafirishaji wa mazao ya bustani (horticulture) pamoja na zana za kisasa za kilimo na umwagiliaji.

‎Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Chongolo amewaalika wawekezaji hao kushiriki katika Maonesho ya Nane Nane 2026, akieleza kuwa maonesho hayo ni jukwaa muhimu linalokutanisha wakulima, wafugaji, wajasiriamali na wadau wa sekta ya kilimo kwa ajili ya biashara, uwekezaji, ubadilishanaji wa teknolojia na uzoefu katika mnyororo mzima wa thamani.

‎Kwa upande wake, Mwenyekiti wa German Agribusiness Alliance, Bw. Frank Karl Nordmann, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa mwaliko huo na kuthibitisha ushiriki wa jopo hilo katika Maonesho ya Nane Nane 2026.

‎Aidha, amebainisha kuwa ushiriki huo utakuwa fursa ya kuanzisha hatua za awali za uwekezaji na biashara nchini Tanzania, hususan katika mazao ya viazi, kokoa, pamoja na mashine na zana za kilimo.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *