
Tume hiyo imetoa wito kwa:
• Kupunguzwa mara moja kwa mvutano wa kisiasa na kurejea katika utekelezaji kamili wa Mkataba wa Amani Uliorejeshwa.
• Kusitishwa mara moja kwa mashambulizi yote ya anga na operesheni za kijeshi katika maeneo ya raia.
• Upatikanaji wa misaada ya kibinadamu bila masharti, kwa usalama na bila vikwazo, ikiwemo uokoaji wa kitabibu.
• Hatua za haraka za kupunguza mvutano ili kuzuia kusambaa zaidi kwa mzozo.
• Uwajibikaji kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu.
• Kuimarishwa kwa ushirikiano wa kikanda na kimataifa ili kuhakikisha kurejea kwa mpito wa kisiasa jumuishi.
Tume hiyo imezitaka nchi washirika wa kikanda na kimataifa kuongeza juhudi za kidiplomasia kwa pamoja ili kuzuia kuzorota zaidi kwa hali, kurejesha siasa za maafikiano, na kuhakikisha kuwa ulinzi wa raia na upatikanaji wa misaada ya kibinadamu vinachukuliwa kama vipaumbele visivyoweza kujadiliwa.