#HABARI: Watu wasiojulikana wamemvamia msaidizi wa shambani Bw. Joseph Madaha usiku wa jana akiwa kwenye makazi yake katika kijiji na Kata ya Tumbi Wilaya ya Tabora na kumpiga kikatili sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumkata sikio moja la kushoto hali iliyomsababishia umauti, ikidaiwa walikuwa wakimtuhumu kutembea na wake za watu, ambapo baada ya tukio hilo wakatokomea kusikojulikana.

Kufuatia tukio hili mara kadhaa tumefanya jitihada za kumtafuta kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Kamishna Msaidizi wa Polisi Constantine Mbogambi ambaye amedai bado hajapokea taarifa ya tukio hilo na akishapokea atafafanua kwa kina huku Maafisa wa jeshi la polisi waliokuwepo kwenye eneo la tukio waliondoka na mwili huo kwa ajili ya taratibu nyingine za kiuchunguzi kabla ya mazishi.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *