#HABARI: Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetenga shilingi bilioni 6.4 kwa ajili ya kuboresha miundombinu na kununua vifaa vya kisasa katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Kampasi ya Songwe.
Naibu Katibu Mkuu, Profesa Daniel Mushi, amebainisha kuwa uwekezaji huo unalenga kuibua wabunifu wa sayansi na kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi hadi kufikia 300 ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira.
Kampasi hiyo iliyopo wilayani Momba, inatajwa kuwa kubwa kuliko zote nchini ikiwa na eneo la zaidi ya ekari 300. Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la DIT, Profesa Ladslaus Mnyone, ameeleza kuwa mwaka 2025 taasisi ililipa fidia ya shilingi milioni 187 kwa wananchi ili kupata ekari 205 za ziada, hatua inayowezesha upanuzi wa miradi ya kimkakati ya elimu na teknolojia mkoani humo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.