Jeshi la Nigeria limeripoti kuwa wanajeshi watano na afisa mmoja wa polisi wameuawa katika shambulizi la kuvizia kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Jeshi la Nigeria jana liliwakomboa mateka 62 katika operesheni tofauti kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Shambulio hilo lilitokea katika jimbo la Zamfara siku ya Jumatatu, ameeleza Msemaji wa jeshi la Nigeria  David Adewusi.

Mamlaka husika za Nigeria hazikutoa maelezo kuhusu kundi lililohusika na shambulizi hilo, lakini zimesema kuwa magaidi wamehusika katiak hujuma hiyo ya kuvizia.

Msemaji wa jehsi la Nigeria ameongeza kuwa: Licha ya shambulio h ilo la kuvizia, jeshi la Nigeria lilijibu kwa ujasiri shambulio hilo nakuzuia madhara zaidi kwa raia wa maeneo ya karibu. 

Shambulio hilo la kuvizia limeripotiwa baada ya wiki jana jeshi la Nigeria kutekeleza oparesheni zake kwa mafanikio dhidi ya wanamgambo wenye silaha ambapo washukiwa watatu walitiwa mbaroni na silaha kunaswa. 

Olanyi Osoba Msemaji mwingine wa jeshi la Nigeria amesema kuwa mateka hao walikombolewa katika msitu wa Muhhaye unaofahamika kama maficho ya maarufu ya kiongozi wa majambazi Kachalla Alti.

” Juhudi zinaendelea ili kuwaunganisha na familia zao mateka waliokombolewa na jeshi. 

Kaskazini mwa Nigeria ni eneo lililoathirika zaidi nchini humo, huku  vitendo vya utekaji nyara unaofanywa na wanamgambo wenye silaha katika maeneo ya kaskazini-magharibi na kaskazini-kati vikiripotiwa kuongezeka katika miezi ya hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *