Hatua hiyo limesema inaweka zaidi ya watu milioni moja katika hatari ya kukosa msaada muhimu wa kuokoa maisha, na kwa mara ya kwanza nchini Nigeria, WFP italazimika kupunguza shughuli zake na kuwafikia watu 72,000 pekee iwapo ufadhili wa haraka hautapatikana.

WFP inasema Nigeria inakabiliwa na moja ya migogoro mibaya zaidi ya njaa katika nyakati za hivi karibuni. Takribani watu milioni 35 wanakadiriwa kukumbwa na uhaba mkubwa na mbaya zaidi wa chakula wakati wa msimu wa upungufu wa chakula wa mwaka 2026, kulingana na takwimu za hivi karibuni za Cadre Harmonisé  sawa na mfumo wa kutathimini hali ya uhakika wachakula (IPC) kwa Afrika ya Magharibi na Kati. 

Kati yao, watu wapatao 15,000 katika jimbo la Borno wako katika hatari ya njaa ya kiwango cha janga cha IPC Daraja la 5, hatua moja kabla ya baa la njaa. Hivi ndivyo viwango vibaya zaidi vya njaa vilivyorekodiwa katika kipindi cha muongo mmoja.

Huu si wakati wa kusitisha msaada

Huu si wakati wa kusitisha msaada wa chakula. Hatua hii itasababisha madhara makubwa ya kibinadamu, kiusalama na kiuchumi kwa watu walio hatarini zaidi ambao wamelazimika kuyahama makazi yao wakitafuta chakula na hifadhi. Suluhu za kibinadamu bado zinawezekana na ni miongoni mwa nguzo za mwisho za uthabiti zinazozuia uhamaji mkubwa wa watu na kuenea kwa mgogoro katika eneo zima. amesema David Stevenson, mkurugenzi wa WFP nchini Nigeria.

WFP imekuwa ikitoa msaada wa chakula kaskazini-mashariki mwa Nigeria tangu mwaka 2015, ikiwafikia karibu wanawake, wanaume na watoto milioni mbili kila mwaka katika maeneo yaliyoathirika zaidi

Kazi ya WFP nchini Nigeria inaunganisha msaada wa dharura na uungaji mkono muhimu wa kusaidia jamii kukabiliana na mishtuko ya chakula na kupunguza utegemezi wa misaada kwa muda mrefu. Suluhisho za ndani za WFP zinaunga mkono uchumi wa ndani kwa kununua msaada huo ndani ya nchi, kuimarisha minyororo ya thamani na kukuza kujitegemea.

Hata hivyo, kurejea kwa vurugu kumeharibu vibaya jamii dhaifu za vijijini, kuwafanya watu kuyahama makazi yao, kuharibu akiba ya chakula, na kuongeza kwa kasi viwango vya kutisha vya njaa na ukosefu wa usalama. Katika kipindi cha miezi minne iliyopita pekee, watu milioni 3.5 wamelazimika kukimbia makazi yao, huku asilimia 80 wakiwa kaskazini mwa nchi.

Viwango vya utapiamlo katika majimbo kadhaa ya kaskazini pia vimezidi kuwa vibaya, vikifikia kiwango cha hatari kubwa.

Rasilimali zimekwisha

Licha ya michango ya ukarimu iliyowezesha WFP kuendelea kutoa msaada wake wa kuokoa maisha kwa walio hatarini zaidi katika miezi ya hivi karibuni, rasilimali hizo chache sasa zimekwisha.

Stevenson  amesema kuwa iwapo WFP haitaweza kuendelea kusaidia watu waliokimbia makazi yao katika kambi, watalazimika kuondoka kwa kukata tamaa ili kujaribu kuishi. Watajaribu kuhama, au wanaweza kujiunga na makundi ya waasi ili kuwalisha wao na familia zao.

 Ili kuendeleza shughuli zake kaskazini-mashariki mwa Nigeria katika kipindi cha miezi sita ijayo, WFP inahitaji kwa dharura dola za Marekani milioni 129. Bila ufadhili huu, shirika hilo liko katika hatari ya kusimamisha kabisa shughuli zake katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *