Sayyed Abdul Malik al-Houthi, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, baadhi ya nchi zinaweka mashinikizo makubwa ya kiuchumi kwa watu wa Yemen kwa kuchelewesha kwa makusudi kuwasili meli na kubainisha kwamba Baraza la Amani la Trump ni kifuniko tu cha satwa na uporaji.

Abdul Malik al-Houthi amesema hayo katika hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka minane ya kuuawa shahidi Saleh al-Sammad, mkuu wa zamani wa Baraza la Siasa la Yemen na kueleza kwamba, watu wa Yemen wamewatoa kafara mashahidi wengi katika miaka iliyopita katika nyanja mbalimbali za uwajibikaji na mapambano dhidi ya “maadui wa Mungu, maadui wa ubinadamu, na maadui wa ukweli,” na kwamba kuuawa shahidi Saleh Al-Samad ni ishara ya dhulma dhidi ya taifa la Yemen na mashahidi wote.

Al-Houthi amesema kwamba, uvamizi na uchokozi dhidi ya Yemen ulifanywa kwa mipango ya Uzayuni na chini ya usimamizi wa Marekani, Uingereza, na Israel, na kwamba muungano wa Saudi Arabia ndio uliosababisha vita hivi.

Akizungumzia mauaji makubwa dhidi ya watoto, wanawake, na wazee katika miji, vijiji, masoko, barabara, na hospitali, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kwamba uhalifu huu unaonyesha kina cha dhulma dhidi ya watu wa Yemen na kwamba lengo lao lilikuwa kusambaratisha azma na irada thabiti ya taifa.

Akizungumzia mipango mipya ya Marekani kama vile “Baraza la Amani la Trump,” amesema kwamba vyeo hivi ni kifuniko tu cha satwa na uporaji.

Al-Houthi amesisitiza udharura wa mataifa ya Kiislamu kuwa makini, kuwa macho, na kujitolea kwa imani yao na utambulisho wa Kiislamu, akisema kwamba njia pekee ya uhuru na mamlaka ya kujitawal ni kusonga mbele kulingana na utambulisho huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *