Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa Marekani na utawala wa Israel zinabeba dhima kwa mashambulizi yaliyo kinyume cha sheria zilizoyafanya dhidi ya taasisi za nyuklia za Iran zinazoendesha shughuli zake kwa malengo ya amani na ya kiraia na pia mashambulizi ya pande mbili hizo dhidi ya umoja wa ardhi na mamlaka ya kujitawala nchi hii.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumatatu, Esmai Baqaei ameeleza kuwa:” Bila shaka tunautambua utawala wa Israel na Marekani kama wahusika wa mashambulizi yaliyo kinyume cha sheria dhidi ya taasisi za nyuklia za Iran zinazoendesha shughuli zake kwa malengo ya kiraia.”

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza haya akijibu swali aliloulizwa na ripota wa shirika la habari la IRNA kuhusu matamshi ya karibuni ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi aliyetamka kuwa hakusema kwamba Iran ilikuwa inataka kumiliki silaha za nyuklia katika ripoti zake  katika jaribio la  kuhalalisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya taasisi za nyuklia za Iran. 

Baqaei amesema, hata  hivyo kutumiwa vibaya na Marekani na nchi tatu za Ulaya ripoti za IAEA kuliwapa kisingizio Israel na Marekani kustafidi na hali hiyo.

Alibainisha kuwa hata Mkurugenzi Mkuu wa IAEA alikiri kwamba hakuna ripoti kutoka wakala huo yeney ushahidi na inayothibitisha kwamba miradi ya nyuklia wa Iran imekengeuka mkondo wake wa amani.

“Katika mazingira kama hayo,ilitarajiwa kwamba wakala wa IAEA ungelaani haraka hatua za Israel na Marekani dhidi taasisi za nyuklia za Iran, amesema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *