#HABARI: Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso, ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Pangani Mkoani Tanga, amemuhakikishia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa zaidi ya shilingi Bilioni 26 alizozitoa kwa Bunda Mjini Mkoani Mara ili kutekeleza miradi ya maji, itafaninikisha upatikanaji wa maji kwa asilimia 100 kabla ya kufika mwaka 2030.

Aweso amebainisha hayo Mbele ya Dkt. Samia na maelfu ya wananchi wa Bunda Mjini, kwenye muendelezo wa kampeni za Dkt. Samia Mkoani humo, akimshukuru pia Dkt. Samia kwa ujasiri wake, maelekezo yake na ufuatiliaji mkubwa katika kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi, salama na ya uhakika.

Mwanasiasa huyo anayesifika kwa usimamizi mzuri wa sekta ya Maji kwenye serikali ya Dkt. Samia ametolea mfano mradi wa maji wa Nyabeho Wilayani humo akisema gharama za mradi huo ni zaidi ya Bilioni 10, ukitoa maji Ziwa Victoria na kuhudumia Mji wa Bunda, akisema kazi kubwa sasa inayosubiriwa ni Uzinduzi wa mradi huo ambapo amemuomba Dkt. Samia kufanya ziara Mkoani humo mara baada ya kuchaguliwa Oktoba 29, 2025 ili kwenda kuuzindua rasmi.

Waziri huyo wa maji kadhalika amesema kabla ya Dkt. Samia kuingia madarakani mwaka 2021, miradi mingi ya maji ilionekana kuwa kichaka cha kuiba fedha kwa watumishi wasiokuwa waaminifu, suala ambalo lilisababisha kukwama kwa miradi mingi ya maji, akisema kwenye serikali ya Dkt. Samia suala hilo limekoma na miradi mingi imekwamuliwa, suala ambalo limewezesha ongezeko la upatikanaji wa maji katika Mikoa mbalimbali nchini.

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *