Ukiwa mfanyabiashara au mteja, umewahi kujiuliza ‘QR Code’ zina umuhimu gani? Meneja Masoko wa ScanCode Tanzania, Cresensia Mbunda, anaeleza kuwa teknolojia hiyo ni nyenzo muhimu inayorahisisha miamala, upatikanaji wa taarifa sahihi na kuongeza uaminifu katika biashara.

Amesema QR Code zinawasaidia wafanyabiashara, taasisi na wateja kufanya malipo kwa urahisi, kupata taarifa muhimu za bidhaa, sambamba na kumlinda mzalishaji na mtumiaji dhidi ya bidhaa bandia au ghushi. Msikilize hapa…

#AzamTVUpdates
✍Warda John
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *