#HABARI: Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na uvuvi imesema inaendelea kutekeleza miradi ya kuimarisha sekta ya ufugaji wa kuku na ndege wafugwao ikiwa ni pamoja na kutoa chanjo ya kuku ili kuongeza mnyororo wa thamani katika eneo hilo linalo tajwa kuwa na umuhimu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tanzani ina uhitaji wa kuku kwa wastani wa tani laki mbili kwa mwaka kutokana na ongezeko la soko la bidhaa hiyo ambalo limekua likiongezeka mara kwa mara.

Licha ya mafanikio hayo zipo jitihada ambazo Serikali imekua ikizifanyia ikiwa ni pamoja na kutoa chanjo kwa ndege aina ya kuku kwa zaidi ya asilimia 98 sasa shabaha kubwa ikilenga kuongeza thamani ya bidhaa hiyo Sokoni.

Akiwa kwenye Maonssho ya 9 ya kimataifa ya kuku na ndege wafuwagao yaliyoanza Oktoba 10 hadi 12, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt Edwin Mhede, ametumia jukwaa hilo kueleza mikakati ya Serikali ya kuendeleza sekta hiyo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *