Ili kutatua changamoto hizi, Timu ya Fedha za Kidijitali ya WHO,  na Wizara ya Afya WHO Kenya, imeanzisha mfumo wa malipo ya kidijitali unaolenga kuhakikisha wahudumu wa afya wanalipwa kwa kasi na kwa uaminifu zaidi. Kupitia mfumo huu, malipo sasa yanafika kwa wahudumu ndani ya saa 72 pekee  hatua kubwa ikilinganishwa na wastani wa siku 15 za awali.

“Zamani tulikuwa tunalipwa, lakini kulikuwa na ucheleweshaji uliotuletea changamoto. Kwa mfumo huu mpya wa kidijitali, malipo yanakuja kwa wakati, na sijawahi kupata matatizo yoyote,” amesema  Joram Obadiah Andera, mhudumu wa afya wa jamii kutoka Kaunti ya Busia.

Ivy Lotilia msimamizi wa kampeni ya utoaji chanjo ya matone ya polio katika kaunti ya West Pokot nchini Kenya akipatia mtoto chanjo ya polio.

UNICEF Kenya

Ivy Lotilia msimamizi wa kampeni ya utoaji chanjo ya matone ya polio katika kaunti ya West Pokot nchini Kenya akipatia mtoto chanjo ya polio.

Kikosi kazi cha kitaifa cha malipo ya kidijitali kiliundwa kuratibu ukusanyaji wa data, usajili wa wahudumu, uthibitishaji wa taarifa na usimamizi wa malipo. Licha ya changamoto za awali kama tofauti za vitambulisho na nambari za simu, mfumo huu umepokelewa vyema kutokana na kasi, usahihi na uwazi wake.

Wizara ya Afya imecheza jukumu muhimu katika kuratibu kati ya kaunti na washirika na kuhakikisha utekelezaji unaenda vizuri. Kenya iko tayari kwa mageuzi ya kidijitali katika utoaji wa huduma za afya,” amesema Sam Siboyi, kiongozi wa fedha za kidijitali, Wizara ya Afya Kenya.

Ushirikiano thabiti na mtoa huduma wa pesa kwa simu M-Pesa umewezesha kufikia maeneo ya mbali zaidi, kuimarisha umiliki wa serikali, na kuonesha mfano unaoweza kuigwa kwa kampeni nyingine za afya.

Mfumo huu ni wa haraka zaidi, sahihi, na umepunguza marudio. Kaunti zimechukua jukumu, na wahudumu wa mstari wa mbele wamehamasishwa kwa sababu wanajua watapokea malipo kwa wakati,” amesema Lucy Murutu, msaidizi wa mpango, WHO Kenya.

Athari za mfumo huu mpya tayari zinaonekana, zaidi ya wahudumu wa afya 120,000 wameandikishwa katika hifadhidata iliyothibitishwa, malipo ambayo hapo awali yalichukua zaidi ya wiki mbili sasa yanakamilika ndani ya siku chache na wafanyakazi 127 wa Wizara ya Afya katika kaunti 13 wamefunzwa kusimamia mchakato huo.

Kwa uwekezaji endelevu, mfumo wa malipo ya kidijitali wa Kenya umeweka msingi wa mageuzi mapana ya ufadhili wa afya, kuhakikisha wahudumu wa mstari wa mbele wanalipwa kwa haraka, kwa usalama na kwa uwazi  na hivyo kuboresha utoaji wa chanjo zinazookoa maisha kote nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *