
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ndege zisizokuwa na rubani kwa siku ya tatu mfululizo, zimeshambulia jiji kuu Khartoum na uwanja wake wa kimataifa wa ndege jijini Khartoum, kwa mujibu wa mashuhuda.
Shuhuda mmoja, amesema, “Nilianza kusikia mashambulio mazito kuanzia saa kumi Alfajiri siku ya Alhamisi, na kuona ndege mbili zikiwa angani zikilenga kambi ya jeshi” ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP.
Aidha, shuhuda mwingine amesema, ameona ndege mbili zisizo na rubani zikielekea kwenye uwanja wa ndege, na baadaye akasikia milipuko, muda mfupi baadaye.
Tangu siku ya Jumanne, uwanja huo wa ndege ambao ulikuwa umefungwa kwa miaka miwili kwa sababu ya vita, umeshuhudia mashambulio mazito kutoka kwa wanamgambo wa RSF.
Uwanja huo ulikuwa ufunguliwe siku ya Jumatano, lakini shughuli hiyo imeahirishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya mwendelezo wa mashambulio yanayoendelea.
Hivi karibuni, serikali inayoongozwa na jeshi, ilikuwa imetangaza kuanza kufunguliwa kwa taasisi na serikali zilizokuwa zimefungwa, baada ya kufanikiwa kudhibiti jiji hilo kubwa miezi kadhaa sasa tangu mwezi Machi.
Vita nchini Sudan kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa RSF, ulioanza Aprili mwaka 2023, umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha wengine zaidi ya Milioni 1 bila makaazi kwa kipindi cha miezi 1O iliyopita.