Wawakilishi kutoka Marekani, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, na Misri watakutana Ijumaa mjini Washington na pande zinazohusika katika mgogoro wa muda mrefu nchini Sudan ili kuzishinikiza kufikia makubaliano ya amani, afisa anayefahamu majadiliano kati ya nchi hizo nne amesema.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliopita, mataifa yenye ushawishi mkubwa ya kigeni, ambayo wakati mwingine hujulikana kama Quad, kwa pamoja yalitoa wito wa makubaliano ya kusitisha mapigano ya kibinadamu nchini Sudan yakifuatiwa na makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano na mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Mkutano wa wiki hii unalenga mpango huo “na kuzishinikiza pande zinazopigana kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano ya kibinadamu ya miezi mitatu nchi nzima,” afisa huyo mwandamizi ameliambia shirika la habari la AFP Alhamisi kwa sharti la kutotajwa jina.

Quad “inafanya kazi kwa pamoja kuweka shinikizo la pamoja kwa pande hizo mbili ili kusimamisha mapigano na kuruhusu misaada kuwafikia raia,” ameongeza.

Afisa huyo amesema wanachama wa kundi hilo watakutana na pande hizo mbili tofauti.

Tangu mwezi Aprili 2023, Sudan imegawanyika kutokana na mapigano kati ya jeshi lake na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).

Mgogoro huo umewaua makumi ya maelfu ya watu na kuwalazimu karibu milioni 12 kutoroka makazi yao, na kusababisha mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi na njaa duniani.

Huku mashahidi wakiripoti ndege zisizo na rubani zikilenga mji mkuu wa Khartoum unaoshikiliwa na jeshi kwa siku ya tatu mfululizo siku ya Alhamisi, mashirika manne ya Umoja wa Mataifa yametoa wito wa “kusitishwa kwa uhasama mara moja.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *