Tehran inakabiliwa na uhaba usio wa kawaida wa maji ya kunywa, tukio mbaya zaidi katika miongo kadhaa. Kwingineko nchini, hakuna tone la maji lililotoka bombanii katika theluthi mbili ya mikoa kwa miezi kadhaa. Kwa hivyo, mji mkuu wa Iran unaweza kulazimika kuhamisha wakazi wake ikiwa mvua haitanyesha mwishoni mwa mwaka, Rais wa Iran Massoud Pezeshkian ameonya katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni siku ya Ijumaa, Novemba 7.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hali inazidi kuwa mbaya kila siku kwa mji mkuu wa Iran na wakazi wake milioni 14 hadi 15, takwimu inayojumuisha miji yote jirai.

Hakuna hata tone moja la mvua lililonyesha tangu msimu uliopita wa masika. Mabwawa yote manne yanayoipa Tehran maji ya kunywa ni tupu, na siku chache tu zimesalia kabla ya kukauka kabisa, anaripoti mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi. Hii ndiyo hali mbaya zaidi katika zaidi ya miaka 60, kulingana na maafisa.

Rais Massoud Pezeshkian alitoa tahadhari siku ya Ijumaa, Novemba 7. “Ikiwa mvua haitanyesha, tutalazimika kusambaza maji kwa mgao huko Tehran kati ya mwisho wa mwezi Novemba na mwanzo wa mwezi Desemba. Na hata kama tutasambaza maji kwa mgao, ikiwa mvua haitanyesha wakati huo, tutaishiwa na maji na tutalazimika kuhama Tehran,” ameeleza, bila kutaja jinsi jiji kuu lenye wakazi zaidi ya milioni 10 litakavyohamishwa. Kauli hii imesababisha ukosoaji, haswa kwenye mitandao ya kijamii. “Na ikiwa hakuna mvua kote nchini, je, tutalazimika kuhamisha idadi yote ya watu? Lakini wapi? Tafuta suluhisho,” aeandika mtumiaji mmoja wa mtandao.

Nchi lazima “ijiandae kwa hali mbaya” 

Akinukuliwa na shirika la habarila serikali la IRNA, mkuu wa kampuni ya maji ya mji mkuu, Behzad Parsa, alionya siku ya  Jumapili kwamba jiji hilo linaweza kukosa maji ya kunywa ndani ya wiki mbili. Bwawa la Amir Kabir, moja kati ya mabwawa matano yanayosambaza maji ya kunywa Tehran, lina “mita za ujazo milioni 14 pekee za maji, au 8% ya uwezo wake,” amesema.

Siku ya Jumatano, mkurugenzi wa kampuni ya maji katika mkoa huo, Mohsen Ardakani, alisisitiza kwenye televisheni ya serikali kwamba wakazi wa Tehran wamepunguza matumizi yake ya maji kwa 10% katika miezi sita iliyopita. “Tukifikia 20%, tutaweza kudumisha hali tulivu kwa mwezi mmoja au miwili, hadi mvua inyeshe,” amesema.

Kulingana na shirika la habari la Tasnim, mvua nchini Iran mwaka huu imeshuka hadi milimita 152, 40% chini ya wastani wa miaka 57 iliyopita. Katika baadhi ya majimbo, mvua imeshuka kwa 50 hadi 80%, Mohammad Reza Kavianpour, mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Maji yenye makao yake makuu Tehran, ameliambia shirika hilo, akiongeza kuwa nchi lazima “ijiandae kwa hali mbaya.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *