
Nchini Sudan, hakuna dalili ya kupungua kwa mapigano kufuatia tangazo la RSF siku ya Alhamisi, Novemba 6, la makubaliano yake ya kusitisha mapigano kwa ajili ya kupiisha misaada ya kibinadamu kwa miezi mitatu.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku ya Ijumaa, Umoja wa Mataifa ulionya kuhusu “maandalizi ya kuongezeka kwa uhasama”. Wimbi la mashambulizi ya ndege zisizo na rubani lililenga miji kadhaa siku ya Ijumaa, ikiwa ni pamoja na Omdurman, karibu na mji mkuu. Jiji la Babnusa huko West Kordofan, lililozingirwa na vikosi vya Jenerali Hemedti, lilikabiliwa na mashambulizi makali ya mizinga.
Wataalamu kadhaa wameelezea mashaka kuhusu nia ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ya kuleta amani. Ripoti kutoka nchini humo zinaonyesha kwamba RSF wanajiandaa kuchukua El Obeid, mji mkuu wa Jimbo la North Kordofan.
Wanamgambo hao hawana nia ya kutekeleza makubaliano haya ya kusitisha mapigano “na badala yake wanajaribu kupotosha umakini kutoka kwa ukatili wanaoufanya huko El-Fasher,” anasema mtafiti Cameron Hudson, mchambuzi katika Kituo cha Mafunzo ya Kimataifa ya Mikakati (CSIS) huko Washington. Bado ana shaka kuhusu uwezekano wa kusitisha mapigano. Jeshi la Sudan halijajibu moja kwa moja wito wa Quartet kwa ajili ya Sudan, inayoundwa na Marekani, Saudi Arabia, Misri, na Falme za Kiarabu.
Uwepo wa UAE katika kundi hili haukubaliwi na jeshi, ambalo linabaini kwamba mtu hawezi kuwa mwamuzi na mshiriki. Ushahidi unaoonekana, uliotolewa na Umoja wa Mataifa, upo kuhusu ushiriki wa Abu Dhabi katika vita nchini Sudan ikisaadia RSF. Khartoum imekataa kushiriki katika mikutano ya hivi karibuni ya Quartet. Jeshi lilirejelea msimamo wake siku ya Alhamisi, Novemba 6, likitangaza kwamba vikosi vyake vitaendelea “kumshinda adui.” Linataka kurejesha kwenye himaya yake majimbi ya Kordofan na Darfur kabla ya mazungumzo yoyote ya amani. Kuhusu raia wa Sudan, wengi wanatilia shaka uzito wa dhamira ya RSF ya amani, hasa baada ya kukiuka makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano hapo awali.
Picha za miili iliyochomwa moto huko El-Fasher
Tangazo la RSF la kukubali amani linakuja huku wanajeshi wa Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana kama Hemedti, wakiendelea na uhalifu wao huko El-Fasher na kwingineko, wakati huu bila kupiga picha, huku ikiwaamuru wanajeshi wake. “Wanamgamo wa RSF wanatupa miili ya wale waliyowaua” wanasema watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani, ambacho ni wa Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu, ambayo huchambua picha za setilaiti kila siku ili kuorodhesha ukatili huo.
Kulingana na Caitlin Howard, picha za setilaiti zilizopigwa katika jiji hilo jiji zinaonyesha wazi kwamba wanamgambo wa RSF “wanasafisha” eneo hilo. “Katika picha za setilaiti, zinaonekana alama za kuungua, nyenzo zilizoungua, moshi … Tunaogopa kwamba vitu tunayoyaona katika picha hizi, tunaamini kuwani miili ya xatu, inayochomwa,” ameielezea RFI.
Kuna maeneo mawili ambapo alama hizi za kuungua zinaonekana. Mojawapo ya maeneo haya ni hospitali ya Saudi Arabia, ambapo inajulikana mauaji yaliyofanyika. Katika picha zetu, tunaona wazi mabaki mengi yaliyoungua, ukubwa wa watu wazima. Eneo la pili ni Mellit Gate, moja ya njia za kutoka jijini zinazodhibitiwa na FSR. Katika picha zilizopigwa siku chache zilizopita, tunaona rundo kubwa la mabaki haya, yanayofanana na miili ya watu. Leo, katika sehemu hiyo, kuna shimo kubwa tu, lililoungua.