Jeshi la polisi linawatafuta viongozi wakuu wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, kwa madai ya kuhusishwa na machafuko makubwa yaliyotokea wiki iliyopita katika miji mbalimbamnali, wakati wa uchaguzi mkuu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada ya polisi kutoa taarifa ya kuwatafuta viongozi wao, baadhi yao tayari wameshakamatwa, akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Tanzania Bara Amani Golugwa ambaye alitiwa mbarano Jumamosi asubuhi.
Mwingine aliyekamatwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Kanda ya Pwani Boniface Jacob maarufu kwa jina la Boni Yai. Ripoti zinasema alikamatwa jijini Dar es Salaam, akiwa njiani kwenda kuripoti polisi.
Wengine wanaotafutwa na polisi ni pamoja na msemaji wa chama hicho, Brenda Rupia, Katibu Mkuu John Mnyika miongoni mwa wengine, akiwemo Mchungaji maarufu na mbunge wa zamani wa Kawe kupitia chama tawala CCM, Josephat Gwajima.

Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amekuwa kizuizini tangu mwezi Aprili ambapo amefunfuliwa kesi ya uhaini, huku naibu wake John Heche naye akikamatwa hivi karibuni na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi.
Haya yanajiri, baada ya siku ya Ijumaa watu zaidi ya 200 kufunguliwa mashtaka ya uhaini, ambayo adhabu yake ni kifo kwa madai ya kuhusika na vurugu ambazo wanaharakati wa haki za binadamu wanasema watu zaidia ya elfu moja, waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi, idadi ambayo hata hivyo haijathibitishwa huku serikali ikiendelea kusalia kimya.