Ukraine inasema watu  zaidi ya 1,400 kutoka mataifa 36 wanaipigania Urusi, kwenye vita vinavyoendelea kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine, Andrii Sybiha, amewataka viongozi wa nchi za Afrika, kuwaonya na kuwazuia raia wake, kutumiwa kama mamluki wa Urusi, katika mzozo ambao utaishia wao kuuawa kwenye uwanja wa vita.

Aidha, amesema waafrika kwenda kupigana nchini Ukraine ni kama kujitakia kifo kwa sababu, watauawa haraka, akiongeza kuwa wanaoipigania Urusi hawadumu hata mwezi mmoja.

Kauli hii imekuja, baada ya Ukraine kusema kuwa, baadhi ya mataifa ya Afrika, yamekiri kuwa raia wake, wamejiunga na kikosi cha Urusi, kinachopigana nchini Ukraine.

Afisa wa jeshi la Ukraine
Afisa wa jeshi la Ukraine © AP – Michael Shtekel

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wiki hii alisema raia wake 17 wenye umri kati ya miaka 20 hadi 39 walikuwa wamesafirishwa nchini Ukraine kushiriki kwenye vita hivyo.

Naye rais wa Kenya William Ruto, alizungumza na mwenzake wa Ukraine, na kumwomba kuwaachia huru, Wakenya waliokamatwa wakiwa mamluki wa Urusi kwenye vita hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *