Zaidi ya watu 200 wameshtakiwa kwa makosa ya uhaini nchini Tanzania, wakili wao pamoja na vyanzo vengine katika idara ya mahakama vimeliambia shirika la habari la AFP.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Watanzania hao wameshtakiwa zikiwa zimepita siku chache baada ya maandamano ya uchaguzi wa urais ambapo upinzani unasema mamia ya waandamanaji waliuawa.

Rais Samia Suluhu Hassan alishinda uchaguzi huo wa Oktoba 29 kwa kupata asilimia 98 za kura zote kulingana na takwimu za tume ya uchaguzi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Upinzani ulizuiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo ambapo umelitaja zoezi hilo kama kichekesho.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa uapisho wake.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa uapisho wake. via REUTERS – PRESIDENTIAL PRESS UNIT

Maandamano yenye vurugu yalishuhudiwa nchini Tanzania siku ya uchaguzi, vyanzo kadhaa vikithibitisha kuwa mamia au hata maelfu ya watu waliuawa kwenye maandamano hayo.

Mamia ya watu walifikishwa mahakamani Ijumaa ya wiki hii jijini Dar Dar es Salaam.

“Watu hawa wote, ambao ni zaidi ya 250 kwa jumla, walishtakiwa kwa kesi tatu tofauti… na wote wanashtakiwa kwa makosa mawili,” wakili Peter Kibatala aliambia AFP siku ya Ijumaa.

“Kosa la kwanza ni kuwa na njama ya kushiriki uhaini. Na kosa la pili ni uhaini wenyewe,” alisema.

Watanzania waliofikishwa mahakamani wanashtakiwa kwa makosa ya uhaini.
Watanzania waliofikishwa mahakamani wanashtakiwa kwa makosa ya uhaini. REUTERS – Emmanuel Herman

Vyanzo kutoka mahakamani viliambia AFP kuwa karibia watu 240 walishtakiwa katika kesi hiyo.

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema kinasema karibia watu 800 waliuawa katika maandamano ya uchaguzi.

Vyanzo vya kidiplomasia na kiusalama navyo vinasema idadi ya waliouawa huenda ikafika elfu moja, vikunga mkono takwimu za Chadema.

Polisi nchini Tanzania pia imesema inawatafuta viongozi wengine wa upinzani ikiwahusisha na vurugu za baada ya uchaguzi.
Polisi nchini Tanzania pia imesema inawatafuta viongozi wengine wa upinzani ikiwahusisha na vurugu za baada ya uchaguzi. REUTERS – Emmanuel Herman

Mamlaka hadi kufikia sasa imektaa kutoa idadi kamili ya watu waliouawa kwenye maandamano hayo.

Aidha siku ya Ijumaa polisi nchini Tanzania ilisema inawatafuta viongozi wa upinzani akiwemo katibu mkuu John Mnyika, naibu wake Amani Golugwa, na Brenda Rupia msemaji wa chama wakihusishwa na vurugu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *