Katika video mpya iliyotolewa siku ya Jumapili, Novemba 9, kiongozi wa upinzani nchini Cameroon, ambaye bado anakataa kutambua ushindi wa Paul Biya katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 12, ametoa makataa kwa serikali, ambayo anaishutumu kwa kufanya “ujambazi wa kiserikali.” Ikiwa wale wote waliokamatwa kuhusiana na mgogoro wa baada ya uchaguzi hawataachiliwa ndani ya saa 48, “watu watajikuta katika hali ya kujihami,” ametishia.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kufuatia wito wake wa maandamano ya kulaani udanganyifu wa uchaguzi, na kisha wito wake wa “kususia shughuli za serikali na kusalia nyumbani” siku chache kabla ya kuapishwa kwa Paul Biya, Issa Tchiroma Bakary anajaribu kufungua sura mpya katika makabiliano yake na serikali huko Yaoundé. Siku tatu baada ya rais kuapishwa kwa muhula wa nane, kiongozi huyo wa upinzani nchini Cameroon, ambaye bado anadai ushindi katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 12 ambapo alitangazwa rasmi kuchukuwa nafasi ya pili, alizungumza tena siku ya Jumapili, Novemba 9.

Katika video, waziri huyo wa zamani, ambaye anakataa kutambua kuchaguliwa tena kwa Paul Biya, anadai tena kwamba anazungumza kama “rais aliyechaguliwa” wa Cameroon na anatoa makataa: bila kutaja mahali alipo, anaipa mamlaka “saa 48” kuwaachilia “bila masharti” wale wote waliokamatwa kuhusiana na mgogoro wa baada ya uchaguzi, akiwashutumu kwa kufanya “ujambazi wa kiserikali” kwa kutekeleza haua ya kuwakamata raia wengi. “Vinginevyo,” anaongeza, “watu watajikuta katika hali ya kujihami.” Issa Tchiroma pia amelaani hali hiyo kama “isiyokubalika, isiyovumilika,” akisema kwamba “kumi, mamia, maelfu ya Wacameroon wanakamatwa, wanafungwa, na kuteswa.”

“Watu kukamatwa kulifanyika ndani ya mfumo wa kudumisha utulivu wa umma,” serikali inajitetea

Ingawa kwa sasa hakuna takwimu rasmi kuhusu idadi ya watu waliokamatwa katika wiki za hivi karibuni nchini, vikundi vya wanasheria vimeundwa ili kutambua na kuwasaidia walioathiriwa. Wanaharakati wa mashirika ya kiraia wanatoa makadirio ya watu 2,000 waliokamatwa—ikiwa ni pamoja na maafisa wa vyama vya siasa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi—na angalau vifo thelathini.

Kujibu tishio lililotolewa na Issa Tchiroma Bakary, Benoît Ndong Soumhet, Waziri kiongozi katika ofisi ya rais na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha CPDM, chama tawala, anakumbusha kwamba “watu kukamatwa kulifanyika katika muktadha wa kudumisha utulivu dhidi ya vitendo vya uharibifu na uporaji.” Kuhusu makataa yaliyotolewa na kiongozi wa upinzani, amesema kwamba “anasubiri kuona ni nguvu gani mgombea huyo, aliyetangazwa rasmi kuwa kuchukuwa nafasi ya pili katika uchaguzi wa rais, “anapanga kutumia kwa kutekeleza tishio lake.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *